More details

Kurugenzi kutoka Idara mbalimbali CCT zimewasilisha mipango ya mwaka 2025

Kurugenzi kutoka Idara mbalimbali katika Jumuiya ya Kikristo Tanzania zimewasilisha mipango ya mwaka 2025 na kuainisha namna ya utekelezaji wa miradi mbalimbali kwa kila idara itakavyokuwa inatekelezwa. Mambo yaliyowasilishwa ni Mipango na Bajeti ya kila idara katika kutekeleza Mpango Mkakati 2024-2028. Katika utendaji wetu wa kazi ni muhimu sana kuzingatia mpango mkakati wetu ambao ndio dira ya kuweza kupima tuliyopanga na kuhakikisha yanaleta matokeo bora na halisi kwa kila idara ili kufikia dhamira na maono ya Taasisi yetu -Katibu Mkuu Jumuiya ya Kikristo Tanzania (Mchg. Can. Dkt. Moses Matonya) #uwajibikaji_na_utendaji_makini