Mafunzo ya ushauri nasaha kwa wakuu wa shule, walimu washauri kutoka shule zilizoko chini ya makanisa wanachama CCT Tar 7&8 Agost 2024
CCT imetoa mafunzo ya ushauri nasaha kwa wakuu wa shule, walimu washauri kutoka shule zilizoko chini ya makanisa wanachama CCT kutoka Kanda ya Maashariki yenye Mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Zanzibar, Tanga na Morogoro.
Mafunzo yamefanyika kwa siku mbili ambapo siku ya kwanza mafunzio yalifanyika kwa walimu wakuu wa shule na Waratibu wa Elimu kutoka makanisa wanachama wa CCT wanaomiliki shule za sekondari na vyuo. Siku ya pili mafunzo yalifanyika kwa walimu kutoka makanisa wanachama wenye shule za Sekondari.
Mafunzo yamelenga walimu kujua namna nzuri na kusaidia kutoa ushauri katika taaluma na Ushauri nasaha kwa wanafunzi ili kulinda watoto katika tabia zao na kuwasaidia katika kufikia malengo yao kwa usahihi. Ikumbukwe tusipowalea watoto katika maadili mema watapotenza ndoto zao.
Mafunzo yamefungwa na Baba Askofu Philipo Mafuja wa Afrika Inland Church Dayosisi ya Pwani ambapo amepongeza zoezi zima la uratibu wa mafunzo hayo na amewashukuru walimu ambao wameweza kushiriki mafunzo haya ya kuwasaidia wanafunzi shuleni/vyuni katika kukabilianana tabia mbovu, utandawazi na changamoto za ajira .