Kambi ya watoto Singida DC ya kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto
Kambi ya watoto Singida DC ya kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto hasa wa kike ambapo jumla ya watoto 60 kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari wamepata mafunzo.
Miongoni mwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vimebainika na kujadiliwa namna ya kujikinga navyo ni ukeketaji, Ulawiti na vipigo.
Mafunzo yametolewa na CCT kupitia idara ya wanawake , watoto na jinsia ambapo mratibu wa Mradi wa kupambana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto, Dada Elizabeth Ngede amewasihi watoto kulinda mienendo yao, kujitunza na kujithamini kupitia mafunzo haya ili na wao waje kuonya maovu kwa kizazi kijacho huko mbeleni wakija kuwa wazazi.
Diwani wa Kata ya Minga Mhe Ibrahimu Mrua amepongeza CCT kwa jitihada hizi za kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa ukeketaji. Amewasihi watoto kukataa kulala na ndugu wanaowatembelea wawapo nyumbani ili kujikinga na vitendo vya kulawitiwa.
Mkuu wa Idara ya Mipango Tathmini na Ufuatiliaji CCT, bwana Urio Ndekirwa amewasihi watoto kujilinda na kwalinda watoto wengine ambao hawajafika kwenye mafunzo, akiwaomba yeyote atakayeona mtu akimfanyia kitendo ambacho sio sahihi atoe taarifa kwa wahusika (waratibu, walimu, dawati la jinsia, viongozi wa dini) ili kupata msaada Zaidi.