Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania-CCT Askofu Dkt. Fredrick Shoo na Katibu Mkuu wa CCT Mch.canon,Dkt.Moses Matonya pamoja na maaskofu wengine kutoka makanisa wanachama ya CCT na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC)wameshiriki katika mkutano ulioandaliwa na Tume ya Kikristo ya huduma za jamii(CSSC). Mkutano huo wa siku mbili uliofanyika Dar -es-salaam ulilenga kujadili utoaji wa huduma endelevu za afya na elimu kwa sasa na kwa miaka ijayo,ili kuweka mikakati bora zaidi ya kukabiliana na changamoto mbalimbali. Kwa zaidi ya miaka 33 CSSC imeendelea kuzisaidia taasisi zaidi ya 1000 za elimu na Afya zilizopo chini ya Makanisa ya CCT na TEC kuendelea kutoa huduma bora katika Jamii