More details

Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wamewasilisha TAMISEMI Mwongozo wa Ufuatiliaji wa Rasilimali za Umma Kwa Wananchi –MURU (Public Expenditure Tracking System -PETS). Lengo kuu la mwongozo huu ni kuisaidia serikali kama mdau mkuu na mwenye dhamana ya uongozi na wadau wengine wa maendeleo. Mwongozo huu umejikita zaidi kwa upana ushirikishwaji wa wananchi kwa ujumla kuwaleta pamoja na kuweza kufuatilia matumizi ya rasilimali za umma. Mwongozo huu umelenga hasa kuhakikisha rasilimali za umma zinatumika ipasavyo ili kuleta matokeo chanya kwa maendeleo na ustawi wa wananchi.